Isaiah 57:1-6

Ibada Ya Sanamu Ya Israeli Iliyo Batili


1 aMwenye haki hupotea,
wala hakuna hata mmoja awazaye hilo moyoni mwake;
watu wanaomcha Mungu huondolewa,
wala hakuna hata mmoja anayeelewa
kuwa wenye haki wameondolewa
ili wasipatikane na maovu.

2 bWale waendao kwa unyofu
huwa na amani;
hupata pumziko walalapo mautini.


3 c“Lakini ninyi:
Njooni hapa, ninyi wana wa wachawi,
ninyi wazao wa wazinzi na makahaba!

4 dMnamdhihaki nani?
Ni nani mnayemcheka kwa dharau,
na kumtolea ndimi zenu?
Je, ninyi si watoto wa waasi,
uzao wa waongo?

5 eMnawaka tamaa katikati ya mialoni
na chini ya kila mti uliotanda matawi;
mnawatoa kafara watoto wenu kwenye mabonde
na chini ya majabali yenye mianya.


6 f“Sanamu zilizo katikati ya mawe laini ya mabondeni ndizo fungu lenu;
hizo ndizo sehemu yenu.
Naam, kwa hizo mmemimina sadaka za vinywaji,
na kutoa sadaka za nafaka.
Katika haya yote,
niendelee kuona huruma?
Copyright information for SwhKC